Anne Boleyn (* 1501 au 1507; † 19 Mei 1536 mjini London) alikuwa mke wa pili kati ya wake sita wa mfalme Henry VIII wa Uingereza. Mtoto wake Elizabeth aliendelea baadaye kuwa malkia Elizabeth I wa Uingereza.
Henry VIII alimpenda Anne alipokuwa bado kijana mdogo. Lakini Anne alikataa kuwa hawara au mpenzi wa mfalme asipoolewa naye. Upendo wake kwa Anne alimsababisha mfalme kutafuta talaka na mke wake wa kwanza Catherine wa Aragon. Alitaka kuachana naye kwa sababu hakumzaa mtoto wa kiume kama mrithi wa mfalme.
Henry alikataliwa kibali cha Papa wa Roma kwa talaka hii akaamua kujitenga na usimamizi wa Papa akajitangaza kuwa mkuu wa kanisa na maaskofu wa kanisa walikubali talaka.
Henry akamwoa Anne mwaka huohuo wa 1532. 1533 akamzaa mtoto wa kwanza aliyekuwa binti Elizabeth. Mfalme alisikitika kumkosa mvulana tena hakushiriki katika ubatizo wa mtoto lakini alimtambua kama mtoto rasmi na mrithi wake.
1534 na 1536 Anne alihariba mimba. Mfalme baada ya kuna ya kwamba hatakuwa na mtoto wa kiume na Anne alianza kuangalia wanawake wengine. Mfalme alianza kutafuta njia za kuachana naye lakini aliogopa talaka ya pili.
Hapo watu wa mazingira wa mfalme walianza kutafuta mashahidi kwa mashtaki ya uwongo ya kuwa Anne alikuwa na mapenzi na watu wengine. Mfalme aliona hii kuwa njia ya kuachana na Anne bila talaka. Kesu ya Anne ilipelekwa mbele ya mahakama akashtakiwa kuvunja ndoa, kufanya mapenzi na kakaye na kupanga kumwua mfalme. Mashtaki yale yote hayakuweza kuthebitishwa lakini mfalme alikaa kimya na mahakama ilitoa hukumu ya mauti.
Anne Boleyn aliuawa tar. 19 Mei 1536. Mfalme Henry VIII alimchukua mnyongaji kutoka Ufaransa kwa nafasi hii; mnyongaji Jean Rombaud alitumia upanga baada ya shoka ya kawaida na kwa njia hii Anne aliweza kufa haraka na bila mateso.
Mfalme aliendelea kumwoa mke wake wa tatu Jane Seymour.
Mtoto wake Elizabeth alikuwa bado mdogo lakini alilelewa mbali na mama na baadaye mke wa sita wa mfalme aliamua kumlea.